Psalms 89

Wimbo Wakati Wa Taabu Ya Kitaifa

(Utenzi Wa Ethani Mwezrahi)


1 aNitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele;
kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako
ujulikane kwa vizazi vyote.

2 bNitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele
na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.


3 cUlisema, “Nimefanya agano na mteule wangu,
nimemwapia mtumishi wangu Daudi,

4 d‘Nitaimarisha uzao wako milele
na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”


5 eEe Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako,
uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.

6 fKwa kuwa ni nani katika mbingu
anayeweza kulinganishwa na Bwana?
Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni
aliye kama Bwana?

7 gKatika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana,
anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

8 hEe Bwana Mwenye Nguvu Zote,
ni nani aliye kama wewe?
Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu,
na uaminifu wako unakuzunguka.


9 iWewe unatawala bahari yenye msukosuko;
wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.

10 jWewe ulimponda Rahabu
Rahabu hapa ina maana jina la Misri kwa fumbo, yaani mwenye majivuno (lakini sio Rahabu wa Yos 2).

kama mmojawapo wa waliochinjwa;
kwa mkono wako wenye nguvu,
uliwatawanya adui zako.

11 lMbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako,
uliuwekea ulimwengu msingi
pamoja na vyote vilivyomo.

12 mUliumba kaskazini na kusini;
Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.

13 nMkono wako umejaa uwezo;
mkono wako una nguvu,
mkono wako wa kuume umetukuzwa.


14 oHaki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;
upendo na uaminifu vinakutangulia.

15 pHeri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,
wanaotembea katika mwanga
wa uwepo wako, Ee Bwana.

16 qWanashangilia katika jina lako mchana kutwa,
wanafurahi katika haki yako.

17 rKwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao,
kwa wema wako unatukuza pembe
Pembe inawakilisha nguvu.
yetu.

18 tNaam, ngao yetu ni mali ya Bwana,
na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.


19 Ulizungumza wakati fulani katika maono,
kwa watu wako waaminifu, ukasema:
“Nimeweka nguvu kwa shujaa,
nimemwinua kijana miongoni mwa watu.

20 uNimemwona Daudi, mtumishi wangu,
na nimemtia mafuta yangu matakatifu.

21 vKitanga changu kitamtegemeza,
hakika mkono wangu utamtia nguvu.

22 wHakuna adui atakayemtoza ushuru,
hakuna mtu mwovu atakayemwonea.

23 xNitawaponda adui zake mbele zake
na kuwaangamiza watesi wake.

24 yUpendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,
kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.

25 zNitauweka mkono wake juu ya bahari,
mkono wake wa kuume juu ya mito.

26 aaNaye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,
Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’

27 abNitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,
aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.

28 acNitadumisha upendo wangu kwake milele,
na agano langu naye litakuwa imara.

29 adNitaudumisha uzao wake milele,
kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.


30 ae“Kama wanae wataacha amri yangu
na wasifuate sheria zangu,

31 kama wakihalifu maagizo yangu
na kutoshika amri zangu,

32 afnitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,
uovu wao kwa kuwapiga,

33 aglakini sitauondoa upendo wangu kwake,
wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.

34 ahMimi sitavunja agano langu
wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.

35 aiMara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu,
nami sitamdanganya Daudi:

36 ajkwamba uzao wake utaendelea milele,
na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;

37 akkitaimarishwa milele kama mwezi,
shahidi mwaminifu angani.”


38 alLakini wewe umemkataa, umemdharau,
umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.

39 amUmelikana agano lako na mtumishi wako,
na umeinajisi taji yake mavumbini.

40 anUmebomoa kuta zake zote,
na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.

41 aoWote wapitao karibu wamemnyang’anya mali zake;
amekuwa dharau kwa jirani zake.

42 apUmeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,
umewafanya watesi wake wote washangilie.

43 aqUmegeuza makali ya upanga wake,
na hukumpa msaada katika vita.

44 Umeikomesha fahari yake,
na kukiangusha kiti chake cha enzi.

45 arUmezifupisha siku za ujana wake,
umemfunika kwa vazi la aibu.


46 asHata lini, Ee Bwana? Utajificha milele?
Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?

47 atKumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka.
Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!

48 auNi mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,
au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.


49 awEe Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni,
ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?

50 axBwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa,
jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,

51 aydhihaka ambazo kwazo adui zako
wamenisimanga, Ee Bwana,
ambazo kwazo wamesimanga
kila hatua ya mpakwa mafuta wako.


52 azMsifuni Bwana milele!
Amen na Amen.
Copyright information for SwhKC